1 Mambo ya Nyakati 3:17 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli, Biblia Habari Njema - BHND Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli, Neno: Bibilia Takatifu Hawa walikuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka: Shealtieli mwanawe, Neno: Maandiko Matakatifu Hawa ndio waliokuwa wazao wa Yekonia aliyekuwa mateka: Shealtieli mwanawe, BIBLIA KISWAHILI Na wana wa Yekonia, huyo aliyechukuliwa mateka; mwanawe Shealtieli, |
Ndipo akasimama Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zake makuhani, na Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na ndugu zake, nao wakaijenga madhabahu ya Mungu wa Israeli, ili kutoa sadaka za kuteketezwa juu yake, kama ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, mtu wa Mungu.
Katika mwaka wa pili wa kufika kwao katika nyumba ya Mungu, huko Yerusalemu, mwezi wa pili, Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, na ndugu zao wengine, makuhani na Walawi, na watu wote, waliotoka katika uhamisho na kufika Yerusalemu, wakaanza; nao wakawaweka Walawi, hao wenye miaka ishirini na waliozidi, ili kuisimamia kazi ya nyumba ya BWANA.
Ndipo akaondoka Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, na Yoshua, mwana wa Yosadaki, wakaanza kuijenga nyumba ya Mungu iliyoko Yerusalemu; na pamoja nao walikuwa manabii wa Mungu, wakiwasaidia.
BWANA asema hivi, Andikeni habari za mtu huyu kwamba hana watoto, kwamba mtu huyu hatafanikiwa siku zake zote; maana hapana mtu katika wazao wake atakayefanikiwa, akiketi katika kiti cha enzi cha Daudi, na kutawala tena katika Yuda.
Na baada ya ule uhamisho wa Babeli, Yekonia akamzaa Shealtieli; Shealtieli akamzaa Zerubabeli;