Hao nao wakapigiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa koo za baba za makuhani na za Walawi; koo za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.
1 Mambo ya Nyakati 26:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wakapigiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo na wakubwa kwa pamoja, kwa kufuata koo za baba zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kila jamaa, bila kujali wingi, ilipiga kura kuchagua lango watakalosimamia. Biblia Habari Njema - BHND Kila jamaa, bila kujali wingi, ilipiga kura kuchagua lango watakalosimamia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kila jamaa, bila kujali wingi, ilipiga kura kuchagua lango watakalosimamia. Neno: Bibilia Takatifu Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. Neno: Maandiko Matakatifu Kura zilipigwa kwa kila lango, kufuatana na jamaa zao, wakubwa kwa wadogo. BIBLIA KISWAHILI Nao wakapigiwa kura kwa ajili ya kila lango, wadogo na wakubwa kwa pamoja, kwa kufuata koo za baba zao. |
Hao nao wakapigiwa kura vile vile, kama ndugu zao wana wa Haruni, machoni pa Daudi mfalme, na Sadoki, na Ahimeleki, na wakuu wa koo za baba za makuhani na za Walawi; koo za baba za mkuu, vile vile kama za nduguye mdogo.
Ndivyo walivyogawanyika kwa kura, wao kwa wao; kwani kulikuwa na wakuu wa patakatifu, na watumishi wa Mungu, wa wana wa Eleazari, na wa wana wa Ithamari pia.
Katika hao zilikuwa zamu za mabawabu, yaani, katika hao wakuu, wenye huduma kama ndugu zao, wa kutumika katika nyumba ya BWANA.
Kura ya lango la mashariki ikamwangukia Meshelemia. Ndipo wakamtupia kura Zekaria mwanawe, mshauri mwenye busara; na kura yake ikamtokea ya kaskazini.