Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

1 Mambo ya Nyakati 23:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Basi Daudi alipokuwa mzee kwa kuishi siku nyingi; alimtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme wa Waisraeli.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Daudi alipokuwa mzee wa miaka mingi, alimtawaza Solomoni mwanawe awe mfalme wa Israeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Daudi alipokuwa mzee wa miaka mingi, alimtawaza Solomoni mwanawe awe mfalme wa Israeli.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Daudi alipokuwa mzee wa miaka mingi, alimtawaza Solomoni mwanawe awe mfalme wa Israeli.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Sulemani mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Daudi alipokuwa mzee aliyeshiba siku, akamfanya Sulemani mwanawe kuwa mfalme juu ya Israeli.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi Daudi alipokuwa mzee kwa kuishi siku nyingi; alimtawaza mwanawe Sulemani awe mfalme wa Waisraeli.

Tazama sura
Tafsiri zingine

1 Mambo ya Nyakati 23:1
12 Marejeleo ya Msalaba  

Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.

Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.

Mfalme Daudi alikuwa mzee, mkongwe katika siku zake, nao wakamfunika nguo, lakini asipate joto.

Je! Bwana wangu mfalme ndiye aliyelitenda jambo hili, bila kutujulisha sisi watumishi wako ni nani atakayeketi katika kiti cha enzi cha bwana wangu mfalme baada yake?

hakika yake nitafanya leo kama vile nilivyokuapia kwa BWANA, Mungu wa Israeli, nikasema, Kwa yakini Sulemani mwanao atamiliki baada yangu, naye ndiye atakayeketi katika kiti changu cha enzi badala yangu.

Basi Sulemani akaketi katika kiti cha enzi cha Daudi baba yake; na ufalme wake ukawa imara sana.

Akawakusanya wakuu wote wa Israeli, pamoja na makuhani na Walawi.

tena katika wana wangu wote (kwani BWANA amenipa wana wengi), amemchagua Sulemani mwanangu ili aketi juu ya kiti cha enzi cha ufalme wa BWANA, juu ya Israeli.

Akafa akiwa mzee sana, mwenye maisha marefu, mali na heshima; naye Sulemani mwanawe akatawala badala yake.

Utafika kaburini mwenye umri mtimilifu, Kama mganda wa ngano ulivyo wakati wake.