Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.
1 Mambo ya Nyakati 22:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Daudi akatoa amri wageni waliokuwa wanaishi katika nchi ya Israeli wakusanyike, naye akawapangia kazi. Akaweka waashi wachonge vizuri mawe ya kujenga nyumba ya Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Daudi akatoa amri wageni waliokuwa wanaishi katika nchi ya Israeli wakusanyike, naye akawapangia kazi. Akaweka waashi wachonge vizuri mawe ya kujenga nyumba ya Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Daudi akatoa amri wageni waliokuwa wanaishi katika nchi ya Israeli wakusanyike, naye akawapangia kazi. Akaweka waashi wachonge vizuri mawe ya kujenga nyumba ya Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote walioishi Israeli, na kutoka miongoni mwao, akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa hiyo Daudi akatoa amri wakusanyike wageni wote waliokuwa wanaishi Israeli, na kutoka miongoni mwao akaweka waashi ili kuchonga mawe kwa ajili ya kujenga nyumba ya Mungu. BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi akaamuru wakusanyike wageni waliokuwa katika nchi ya Israeli; akaweka waashi wachonge mawe ili kujenga nyumba ya Mungu. |
Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.
Na nyumba ilipokuwa ikijengwa, ikajengwa kwa mawe yaliyokwisha kuchongwa machimboni; wala nyundo, wala shoka, wala chombo cha chuma chochote, sauti yake haikusikiwa ilipokuwa ikijengwa nyumba.
na hao waashi, na wakata mawe, tena kununua miti na mawe ya kuchongwa, ili kuyatengeneza mabomoko ya nyumba ya BWANA, tena kwa gharama zote za kuitengeneza nyumba.
wapewe maseremala, na wajenzi, na waashi; ili kununua miti na mawe yaliyochongwa wapate kuitengeneza nyumba.
Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba.
Kisha mfalme Daudi akawaambia kusanyiko lote, Sulemani mwanangu, ambaye Mungu amemchagua peke yake, angali ni mchanga bado na hana uzoefu, nayo kazi hii ni kubwa; kwani nyumba hii ya enzi si kwa mwanadamu, ila kwa BWANA, Mungu.
nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaipeleka Yerusalemu.
Ndipo Sulemani akawahesabu wageni wote waliokuwamo katika nchi ya Israeli, kulingana na hesabu aliyoifanya Daudi baba yake; wakatokea elfu mia moja hamsini na tatu, na mia sita.
Tena waliwapa waashi na maseremala fedha; wakawapa watu wa Sidoni, na watu wa Tiro, chakula, na vinywaji, na mafuta, ili walete mierezi kutoka Lebanoni mpaka Yafa kwa njia ya bahari, kwa kadiri walivyopewa ruhusa na Koreshi, mfalme wa Uajemi.
kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.