uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;
1 Mambo ya Nyakati 22:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike Torati ya BWANA, Mungu wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu akupe busara na akili ili atakapokupa uongozi juu ya Israeli, uzishike sheria zake Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu akupe busara na akili ili atakapokupa uongozi juu ya Israeli, uzishike sheria zake Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu akupe busara na akili ili atakapokupa uongozi juu ya Israeli, uzishike sheria zake Mwenyezi-Mungu, Mungu wako. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika Torati ya Mwenyezi Mungu, Mungu wako. Neno: Maandiko Matakatifu bwana na akupe hekima na ufahamu wakati atakuweka juu ya Israeli, ili uweze kuishika Torati ya bwana Mwenyezi Mungu wako. BIBLIA KISWAHILI BWANA na akupe busara na akili, akakuagizie juu ya Israeli; ili uishike Torati ya BWANA, Mungu wako. |
uyashike mausia ya BWANA, Mungu wako, uende katika njia zake, uzishike sheria zake, na amri zake, na hukumu zake, na shuhuda zake, sawasawa na ilivyoandikwa katika Torati ya Musa, upate kufanikiwa katika kila ufanyalo, na kila utazamako;
Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwatawala watu wako hawa walio wengi?
kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.
Zishikeni basi, mkazitende, maana hii ndiyo hekima yenu na akili zenu, machoni pa mataifa watakaozisikia amri hizi zote, nao watasema, Hakika taifa hili kubwa ni watu wenye hekima na akili.
Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.