1 Mambo ya Nyakati 2:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na wana wa Karmi; Akani, yule aliyewataabisha Israeli, kwa kuchukua kilichowekwa wakfu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwana wa Karmi, alikuwa Akari. Huyu aliwaletea Waisraeli taabu kwa sababu alijiwekea nyara zilizokuwa zimewekwa wakfu. Biblia Habari Njema - BHND Mwana wa Karmi, alikuwa Akari. Huyu aliwaletea Waisraeli taabu kwa sababu alijiwekea nyara zilizokuwa zimewekwa wakfu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwana wa Karmi, alikuwa Akari. Huyu aliwaletea Waisraeli taabu kwa sababu alijiwekea nyara zilizokuwa zimewekwa wakfu. Neno: Bibilia Takatifu Mwana wa Karmi alikuwa: Akari, ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutochukua vitu vilivyotengwa kwa ajili ya kuangamizwa. Neno: Maandiko Matakatifu Mwana wa Karmi alikuwa: Akari, ambaye alileta taabu kwa Waisraeli kwa kukiuka onyo la kutokuchukua vitu vilivyokuwa vimewekwa wakfu. BIBLIA KISWAHILI Na wana wa Karmi; Akani, yule aliyewataabisha Israeli, kwa kuchukua kilichowekwa wakfu. |
Kisishikamane na mkono wako kitu chochote katika kitu kilichoharimishwa; ili ageuke BWANA na ukali wa hasira zake akurehemu, akuonee huruma, na kukufanya kuwa wengi, kama alivyowaapia baba zako;
na usitie kitu kilicho haramu ndani ya nyumba yako, usije ukalaaniwa kama haramu hiyo; ukichukie kabisa na kukikataa kabisa, kwa kuwa ni kitu kilicholaaniwa.
Je! Huyo Akani mwana wa Zera hakukosa katika vile vitu vilivyowekwa wakfu, na hasira ikauangukia mkutano wote wa Israeli? Kisha mtu huyo hakuangamia peke yake katika uovu wake?
Na ninyi, msikose kujiepusha na kitu kilichowekwa wakfu; msije mkakitwaa kitu kilichowekwa wakfu, baada ya kukiweka wakfu; nanyi hivyo mtaifanya kambi ya Israeli kuwa imelaaniwa na kuifadhaisha.
Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? BWANA atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.