Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mnara wa ukumbusho kwenye mto wa Frati.
1 Mambo ya Nyakati 18:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akapiga katika hao Washami watu elfu ishirini na mbili. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nao Waaramu wa Damasko, walipokwenda kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi aliwashambulia na kuwaua watu 22,000. Biblia Habari Njema - BHND Nao Waaramu wa Damasko, walipokwenda kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi aliwashambulia na kuwaua watu 22,000. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nao Waaramu wa Damasko, walipokwenda kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi aliwashambulia na kuwaua watu 22,000. Neno: Bibilia Takatifu Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua watu elfu ishirini na mbili miongoni mwao. Neno: Maandiko Matakatifu Waaramu wa Dameski, walipokuja kumsaidia Hadadezeri mfalme wa Soba, Daudi akawashambulia na kuwaua 22,000 miongoni mwao. BIBLIA KISWAHILI Na Washami wa Dameski walipokuja wamsaidie Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akawapiga katika hao Washami watu elfu ishirini na mbili. |
Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mnara wa ukumbusho kwenye mto wa Frati.
Daudi akampokonya magari elfu moja, na wapanda farasi elfu saba, na askari waendao kwa miguu elfu ishirini; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila wa magari mia moja akawaweka.
Ndipo Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski; nao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye BWANA akampa Daudi kushinda kila alikokwenda.
Na wana wa Amoni walipoona ya kuwa wamejisababishia machukizo kwa Daudi, Hanuni na wana wa Amoni wakatuma talanta elfu moja za fedha ili kukodi magari na wapanda farasi kutoka Mesopotamia, na kutoka Atam-maaka, na kutoka Soba.
Basi Sauli alipokwisha kuutwaa ufalme juu ya Israeli, alipigana na adui zake wote pande zote, juu ya Moabu, na juu ya wana wa Amoni, na juu ya Edomu, na juu ya wafalme wa Soba, na juu ya Wafilisti; na popote alipogeukia, akawashinda.