basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako.
1 Mambo ya Nyakati 16:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mpeni shukrani Mwenyezi-Mungu, tangazeni ukuu wake, yajulisheni mataifa mambo aliyoyatenda! Biblia Habari Njema - BHND Mpeni shukrani Mwenyezi-Mungu, tangazeni ukuu wake, yajulisheni mataifa mambo aliyoyatenda! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mpeni shukrani Mwenyezi-Mungu, tangazeni ukuu wake, yajulisheni mataifa mambo aliyoyatenda! Neno: Bibilia Takatifu Mshukuruni Mwenyezi Mungu, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. Neno: Maandiko Matakatifu Mshukuruni bwana, liitieni jina lake; wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda. BIBLIA KISWAHILI Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Wajulisheni watu matendo yake. |
basi, usikie huko mbinguni, makao yako, ukatende kwa kadiri ya yote atakayokuomba mgeni huyo; ili watu wote wa dunia wapate kulijua jina lako, na kukucha wewe kama watu wako Israeli, nao wajue ya kuwa nyumba hii, niliyoijenga, imeitwa kwa jina lako.
Basi sasa, Ee BWANA, Mungu wetu, utuokoe na mkono wake, nakusihi, ili kwamba falme zote za dunia zipate kujua ya kuwa wewe ndiwe BWANA Mungu, wewe peke yako.
Na katika siku hiyo mtasema, Mshukuruni BWANA, liitieni jina lake; Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa, Litangazeni jina lake kuwa limetukuka.
itasikika tena sauti ya furaha na sauti ya shangwe, sauti ya bwana arusi na sauti ya bibi arusi, sauti yao wasemao Mshukuruni BWANA wa majeshi, maana BWANA ni mwema, rehema zake ni za milele; na sauti zao waletao sadaka za shukrani nyumbani kwa BWANA. Kwa kuwa nitawarudisha wafungwa wa nchi hii kama kwanza, asema BWANA.
kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, wale waliotakaswa katika Kristo Yesu, walioitwa wawe watakatifu, pamoja na wote wanaoliitia jina la Bwana wetu Yesu Kristo kila mahali, Bwana wao na wetu.