Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi.
1 Mambo ya Nyakati 16:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Metithia, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alimchagua Asafu kuwa kiongozi wao, akisaidiwa na Zekaria. Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Metithia, Eliabu, Benaya, Obed-edomu na Yehieli, aliwachagua wawe wapiga vinanda na vinubi. Asafu alipiga matoazi, Biblia Habari Njema - BHND Alimchagua Asafu kuwa kiongozi wao, akisaidiwa na Zekaria. Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Metithia, Eliabu, Benaya, Obed-edomu na Yehieli, aliwachagua wawe wapiga vinanda na vinubi. Asafu alipiga matoazi, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alimchagua Asafu kuwa kiongozi wao, akisaidiwa na Zekaria. Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Metithia, Eliabu, Benaya, Obed-edomu na Yehieli, aliwachagua wawe wapiga vinanda na vinubi. Asafu alipiga matoazi, Neno: Bibilia Takatifu Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, Neno: Maandiko Matakatifu Asafu ndiye alikuwa mkuu wao, akisaidiwa na Zekaria, Yeieli, Shemiramothi, Yehieli, Matithia, Eliabu, Benaya, Obed-Edomu na Yeieli. Hawa ndio wangepiga zeze na vinubi, Asafu angepiga matoazi, BIBLIA KISWAHILI Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Metithia, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi; |
Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za BWANA kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi.
Basi akawaacha huko, mbele ya sanduku la Agano la BWANA, Asafu na nduguze, ili watumike mbele ya sanduku daima, kila siku kama ilivyokuwa kazi yake.
Akawaagiza baadhi ya Walawi kwamba watumike mbele ya sanduku la BWANA, wamfanyie ukumbusho, na shukrani, na sifa, BWANA, Mungu wa Israeli;
nao makuhani Benaya na Yahazieli wenye baragumu daima, mbele ya sanduku la Agano la Mungu.
na mwanawe huyo ni Tahathi, na mwanawe huyo ni Urieli, na mwanawe huyo ni Uzia, na mwanawe huyo ni Shauli.
Na nduguye Asafu, aliyesimama upande wake wa kulia, huyo Asafu alikuwa mwana wa Berekia, mwana wa Shimea;
Akawasimamisha Walawi nyumbani mwa BWANA wenye matoazi, wenye vinanda, na wenye vinubi, kama alivyoamuru Daudi, na Gadi mwonaji wa mfalme, na Nathani nabii; kwani BWANA aliamuru hivi kwa manabii wake.