1 Mambo ya Nyakati 16:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Yakumbukeni matendo yake yote ya ajabu aliyoyafanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, maajabu yake na hukumu alizotoa, Biblia Habari Njema - BHND Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, maajabu yake na hukumu alizotoa, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kumbukeni matendo ya ajabu aliyotenda, maajabu yake na hukumu alizotoa, Neno: Bibilia Takatifu Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, Neno: Maandiko Matakatifu Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya, miujiza yake na hukumu alizozitamka, BIBLIA KISWAHILI Yakumbukeni matendo yake yote ya ajabu aliyoyafanya; Miujiza yake na hukumu za kinywa chake; |
Kicho cha BWANA ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za BWANA ni kweli, Zina haki kabisa.
Kisha itakuwa hapo mwanao atakapokuuliza kesho, akisema, Ni nini hivi? Utamwambia, BWANA alimtoa Misri, kutoka ile nyumba ya utumwa, kwa uwezo wa mkono wake;
Musa akawaambia hao watu, Kumbukeni siku hii, mliyotoka nchi ya Misri, kutoka nyumba ya utumwa; kwa kuwa BWANA aliwatoa mahali hapa kwa nguvu za mkono wake; na usiliwe mkate uliochachwa.
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Hukumu zake hazichunguziki, wala njia zake hazieleweki!
Nikaisikia hiyo madhabahu ikisema, Naam, Bwana Mungu Mwenyezi, hukumu zako ni za kweli, na haki.
kwa kuwa hukumu zake ni za kweli na haki; maana amemhukumu yule kahaba mkuu aliyeiharibu nchi kwa uasherati wake, na kuipatiliza damu ya watumwa wake mkononi mwake.