1 Mambo ya Nyakati 14:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wafilisti walipokimbia, waliziacha sanamu za miungu yao huko, naye Daudi akatoa amri zote zichomwe moto. Biblia Habari Njema - BHND Wafilisti walipokimbia, waliziacha sanamu za miungu yao huko, naye Daudi akatoa amri zote zichomwe moto. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wafilisti walipokimbia, waliziacha sanamu za miungu yao huko, naye Daudi akatoa amri zote zichomwe moto. Neno: Bibilia Takatifu Wafilisti walikuwa wametupa miungu yao huko, naye Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto. Neno: Maandiko Matakatifu Wafilisti walikuwa wameacha miungu yao huko, Daudi akaamuru iteketezwe kwa moto. BIBLIA KISWAHILI Nao wakaiacha miungu yao huko; naye Daudi akaamuru, ikateketezwa kwa moto. |
na kuitupa miungu yao motoni; kwa maana haikuwa miungu, bali ni kazi ya mikono ya wanadamu; ilikuwa miti na mawe tu, ndiyo sababu wakaiharibu.
Basi wakapanda mpaka Baal-perasimu, Daudi naye akawapiga huko; Daudi akasema, BWANA amewafurikia adui zangu kwa mkono wangu, kama mafuriko ya maji. Basi wakapaita mahali pale jina lake Baal-perasimu.
Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawaua wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi BWANA.
Akaitwaa ile ndama waliyoifanya, akaichoma moto, akaisaga hata ikawa mavumbi, akainyunyiza juu ya maji, akawanywesha wana wa Israeli.
Sanamu za kuchonga za miungu yao mtaziteketeza kwa moto; usitamani fedha wala dhahabu iliyo juu yao, wala usiitwae iwe yako usije ukanaswa nayo; kwa maana ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako;
Lakini watendeni hivi; zivunjeni madhabahu zao zibomoeni nguzo zao, yakateni maashera yao, ziteketezeni kwa moto sanamu zao za kuchonga.