na hao Wabeerothi walikimbia kwenda Gitaimu, ndipo wanapokaa kama wageni hata hivi leo.)
1 Mambo ya Nyakati 13:13 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Basi Daudi hakujichukulia sanduku mjini mwa Daudi, ila akalihamisha kando na kulitia nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Basi, Daudi hakulichukua sanduku mpaka mji wa Daudi, bali alilipeleka nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. Biblia Habari Njema - BHND Basi, Daudi hakulichukua sanduku mpaka mji wa Daudi, bali alilipeleka nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Basi, Daudi hakulichukua sanduku mpaka mji wa Daudi, bali alilipeleka nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. Neno: Bibilia Takatifu Hakulichukua hilo Sanduku akae nalo katika Mji wa Daudi. Badala yake, akalipeleka nyumbani mwa Obed-Edomu, Mgiti. Neno: Maandiko Matakatifu Hakulichukua hilo Sanduku akae nalo katika Mji wa Daudi. Badala yake, akalipeleka nyumbani kwa Obed-Edomu, Mgiti. BIBLIA KISWAHILI Basi Daudi hakujichukulia sanduku mjini mwa Daudi, ila akalihamisha kando na kulitia nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. |
na hao Wabeerothi walikimbia kwenda Gitaimu, ndipo wanapokaa kama wageni hata hivi leo.)
na pamoja nao ndugu zao kwa cheo cha pili, Zekaria, na Yaasieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Uni, na Eliabu; na Benaya, na Maaseya, na Matithia, na Elifelehu, na Mikneya, na Obed-edomu, na Yeieli, mabawabu.
Basi Daudi, na wazee wa Israeli, na makamanda wa maelfu, wakaenda, ili kulipandisha sanduku la Agano la BWANA kutoka nyumbani mwa Obed-edomu kwa furaha kuu;
Asafu mkuu wao, na wa pili wake Zekaria, na Yeieli, na Shemiramothi, na Yehieli, na Metithia, na Eliabu, na Benaya, na Obed-edomu, na Yeieli, wenye vinanda na vinubi; naye Asafu mwenye kupiga matoazi;
Naye Obed-edomu alikuwa na wana; Shemaya mzaliwa wa kwanza, Yehozabadi wa pili, Yoa wa tatu, na Sakari wa nne, na Nethaneli wa tano;
Hao wote walikuwa wana wa Obed-edomu; wao na wana wao na ndugu zao, watu hodari wawezao huo utumishi; watu wa Obed-edomu sitini na wawili.