Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
1 Mambo ya Nyakati 1:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. Biblia Habari Njema - BHND Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lameki akamzaa Noa. Noa alikuwa na wana watatu: Shemu, Hamu na Yafethi. Neno: Bibilia Takatifu Wana wa Nuhu walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi. Neno: Maandiko Matakatifu Wana wa Nuhu walikuwa: Shemu, Hamu na Yafethi. BIBLIA KISWAHILI na Nuhu, na Shemu, na Hamu, na Yafethi. |
Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika.
BWANA akamwambia Nuhu, Ingia wewe na jamaa yako yote katika safina; kwa maana nimekuona wewe u mwenye haki mbele zangu katika kizazi hiki.
Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani.
Wana wa Yafethi; Gomeri, na Magogu, na Madai, na Yavani, na Tubali, na Mesheki, na Tirasi.
wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao, asema Bwana MUNGU.
Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu katika habari za mambo yasiyoonekana bado, kwa jinsi alivyomcha Mungu, aliunda safina, apate kuiokoa nyumba yake. Na hivyo akauhukumu makosa ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.
wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;