akageuka sura yake mbele yao: uso wake ukangʼaa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
Ufunuo 19:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921 Nae alipewa kuvikwa kwa katani safi, ya fakhari, kwa maana katani hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu). Biblia Habari Njema - BHND Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu). Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Amepewa uwezo wa kujivalia nguo ya kitani safi, iliyotakata na yenye kung'aa!” (Nguo hiyo ya kitani safi ni matendo mema ya watakatifu). Neno: Bibilia Takatifu Akapewa kitani safi, inayong’aa na nzuri, ili avae.” (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.) Neno: Maandiko Matakatifu Akapewa kitani safi, nyeupe inayong’aa, ili avae.” (Hiyo kitani safi inawakilisha matendo ya haki ya watakatifu.) BIBLIA KISWAHILI Naye ameruhusiwa kuvikwa kitani nzuri, ing'aayo, safi; kwa maana kitani nzuri hiyo ni matendo ya haki ya watakatifu. |
akageuka sura yake mbele yao: uso wake ukangʼaa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.
akageuka sura yake mbele yao: mavazi yake yakawa yakimetameta, meupe kwa mfano wa thuluji, jinsi asivyoweza fundi duniani kuyafanya meupe.
Ikawa wangali wakishangaa kwa haya, kumbe! watu wawili wakisimama karibu yao, wamevaa nguo za kumetameta.
Walipokuwa wakikaza macho mbinguni, yeye alipokuwa akienda zake, watu wawili wakasimama karibu nao, wenye nguo nyeupe,
ni haki ya Mungu, ipatwayo kwa kuwa na imani kwa Yesu Kristo, huja kwa watu wote, huwakalia watu wote waaminio.
Ni nani asiyekucha, Bwana, na kulitukuza jina lako? kwa kuwa wewe peke yako Mtakatifu: kwa maana mataifa yote watakuja na kusujudu mbele yako; kwa kuwa matendo yako ya haki yamekwisha kufunuliwa.
na wale malaika saba, wenye mapigo saba, wakaloka katika hekalu, wamevikwa mavazi ya kitani safi, kingʼaacho, wamefungwa vifuani mwao mishipi ya dhahabu.
Na majeslii yaliyo mbinguni yakamfuata, wamepanda farasi weupe na kuvikwa katani safi, nyeupe.
Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri; na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya nchi wako isionekane; na dawa ya macho ya kujipaka macho yako upate kuona,