Mathayo 24:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921 Na kama siku zile zisingalikatizwa, asingeokoka mtu ye yote; lakini kwa ajili ya wateule zitakatizwa siku zile. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa. Biblia Habari Njema - BHND Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Kama siku hizo hazingalipunguzwa, hakuna binadamu yeyote ambaye angeokoka; lakini siku hizo zitapunguzwa kwa ajili ya wale walioteuliwa. Neno: Bibilia Takatifu “Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna mtu ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupishwa. Neno: Maandiko Matakatifu Kama siku hizo zisingefupishwa, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeokoka. Lakini kwa ajili ya wateule, siku hizo zitafupizwa. BIBLIA KISWAHILI Na kama siku hizo zisingalifupishwa, asingeokoka mtu yeyote; lakini kwa ajili ya wateule siku hizo zitafupishwa. |
Kwa maana wataondoka Makristo ya uwongo, na manabii ya uwongo, nao watafanyiza ishara kubwa ua mataajabu; wapate kuwadanganya, kama yumkini, hatta wateule.
Nae atawatuma malaika zake pamoja na sauti kuu ya panda, nao watawakusanya wateule wake toka pepo nne, toka upande mmoja wa mwisho wa mbinguni mpaka upande wa pili.
Na kama Bwana asingalizikatiza siku zile, asingeokoka mtu aliye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku zile.
Bassi Mungu je! hatawapatia haki wateule wake wanaomlilia mchana na usiku, nae ni mvumilivu kwao? Nawaambieni atawapatia haki upesi.
kwa maana kabla hawajazaliwa wale watoto, wala hawajatenda neno jema wala baya, illi lisimame kusudi la Mungu la kuchagua,
Kwa ajili ya hilo nastahimili yote, kwa ajili ya wateule, wao nao waupate wokofu ulio katika Kristo Yesu pamoja ua utukufu wa milele.
PETRO, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Mtawanyiko, wakaao bali ya wageni katika Ponto, Galatia, Kappadokia, Asia na Bithunia,