Mathayo 24:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921 Bassi mlionapo chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama mahali patakatifu (asomae afahamu), Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake), Biblia Habari Njema - BHND “Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake), Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Basi, mtakapoona ‘Chukizo Haribifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu, (msomaji na atambue maana yake), Neno: Bibilia Takatifu “Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu), Neno: Maandiko Matakatifu “Hivyo mtakapoona lile ‘chukizo la uharibifu’ lililonenwa na nabii Danieli limesimama mahali patakatifu (asomaye na afahamu), BIBLIA KISWAHILI Basi hapo mtakapoliona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Danieli, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu), |
Lakini mlionapo chukizo la uharibifu (lile lililoneuwa ua nabii Danieli) likisimama pasipolipasa (asomae na afahamu) ndipo walio katika Yahudi wakimbilie milimani;
Kwa maana siku zitakujilia, adui zako watakapokujengea boma; watakuzunguka, watakudhiikisha pande zote;
Lakini, mtakapoona Yerusalemi unazungukwa na majeshi, ndipo jueni ya kuwa uharibifu wake umekaribia.
Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini: na Warumi watakuja, wataondoa mahali petu na taifa letu.
Huyu ndiye mtu yule afundishae watu katika killa mahali kinyume cha taifa letu na torati na pahali hapa. Tena, zaidi ya haya, amewaingiza Wayunani katika hekalu, akapatia najis pahali hapa palakatifu.
Wakasimamisha mashahidi wa uwongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati:
Yu kheri asomae, nao wayasikiao maneno ya unabii huu na kuyafanya yaliyoandikwa humo: maana wakati ni karibu.