Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.
Mathayo 12:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921 Na Shetani akimfukuza Shetani, amefitinika na nafsi yake; bassi ufalme wake utasimamaje? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, anajipinga mwenyewe. Basi, ufalme wake utasimamaje? Biblia Habari Njema - BHND Ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, anajipinga mwenyewe. Basi, ufalme wake utasimamaje? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ikiwa Shetani anamfukuza Shetani, anajipinga mwenyewe. Basi, ufalme wake utasimamaje? Neno: Bibilia Takatifu Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama? Neno: Maandiko Matakatifu Kama Shetani akimtoa Shetani, atakuwa amegawanyika yeye mwenyewe. Basi ufalme wake utawezaje kusimama? BIBLIA KISWAHILI Na Shetani akimtoa Shetani, amefitinika juu ya nafsi yake; basi ufalme wake utasimamaje? |
Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.
Ndipo Yesu akamwambia, Nenda zako, Shetani: kwa maana imeandikwa, Utamsujudia Bwana Mungu wako, nae peke yake utamwabudu.
Sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana mkuu wa ulimwengu anakuja, wala hana kitu kwangu:
ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
aliyetuokoa na uguvu za giza, akatuhamisha na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wa pendo lake;
Joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwae Msingiziaji na Shetani, audanganyae ulimwengu wote; akatupwa hatta inchi, na malaika zake wakatupwa pamoja nae.
Malaika wa tano akakimimina kichupa chake juu ya kiti cha enzi cha yule nyama, ufalme wake ukatiwa giza, wakatafuna ndimi zao kwa sababu ya maumivu yao,
Na juu yao wana mfalme, malaika wa abuso, jina lake kwa Kiebrania Abaddon, na kwa Kiyunani jina lake Apollion.