mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.
Mathayo 11:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921 IKAWA Yesu alijiokwisha kuwaagiza wanafunzi wake thenashara, akatoka huka kwenda kufundisha na kukhubiri katika miji yao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Yesu alipomaliza kuwapa wanafunzi kumi na wawili maagizo, alitoka hapo, akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Biblia Habari Njema - BHND Yesu alipomaliza kuwapa wanafunzi kumi na wawili maagizo, alitoka hapo, akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Yesu alipomaliza kuwapa wanafunzi kumi na wawili maagizo, alitoka hapo, akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. Neno: Bibilia Takatifu Baada ya Isa kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji ya Galilaya. Neno: Maandiko Matakatifu Baada ya Isa kumaliza kutoa maagizo kwa wanafunzi wake kumi na wawili, aliondoka hapo akaenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. BIBLIA KISWAHILI Ikawa Yesu alipokwisha kuwaagiza wanafunzi wake kumi na wawili, alitoka huko kwenda kufundisha na kuhubiri katika miji yao. |
mkiwafundisha kushika yote niliyowaamuru ninyi: nti tazama, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hatta mwisho wa dunia. Amin.
Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.
Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.
Nao wakamshurutisha, wakisema, Awataharakisha watu, akifundisha katika Yahudi yote, akianzia Galilaya hatta hapa.
IKAWA muda si muda alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji, akikhutubu na kukhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu. Na wale thenashara walikuwa pamoja nae,
Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama mimi nilivyozishika amri za Baba yangu, na kukaa katika pendo lake.
khabari za Yesu wa Nazareti, jinsi Mungu alivyomtia mafuta kwa Roho Mtakatifu na uguvu: nae akatembea huko na huko, akitenda kazi njema na kuponya wote walioonewa na Shetani; kwa maana Mungu alikuwa pamoja nae.
Akatuagiza tuwakhubiri watu na kushuhudu ya kuwa huyu udiye aliyeamriwa na Mungu awe Mhukumu wa hayi na wafu.
Kwa maana hatta wakati ule tulipokuwapo kwenu tuliwaagiza neno hili, kwamba ikiwa mtu hataki kufanya kazi, bassi, asile chakula.
Twawaagizeni, ndugu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, jitengeni nafsi zenu na killa ndugu aendae bila utaratibu, wala si kwa kufuata mapokeo mliyoyapokea kwetu.
ilinde amri hii pasipo mawaa, pasipo lawama, hatta kudhihiri kwake Bwana wetu Yesu Kristo,