Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.
2 Wakorintho 4:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921 ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu. Biblia Habari Njema - BHND Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hao hawaamini kwa sababu yule mungu wa ulimwengu huu amezitia giza akili zao wasipate kuuona wazi mwanga wa Habari Njema ya utukufu wa Kristo, ambaye ni mfano kamili wa Mungu. Neno: Bibilia Takatifu Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Al-Masihi, aliye sura ya Mungu. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa habari yao, mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, ili wasione nuru ya Injili ya utukufu wa Al-Masihi, aliye sura ya Mungu. BIBLIA KISWAHILI ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, wasiione nuru ya Injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. |
Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.
Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.
Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote, Mwana wa pekee aliye katika kifua cha Baba, huyu ndiye aliyefasiri khabari yake.
Bassi Yesu akawaambia, Nuru ingali pamoja nanyi muda kitambo. Enendeni maadam mnayo ile nuru, giza lisije likawaweza; nae aendae gizani hajui aendako.
Amewapofusba macho, amefanya migumu mioyo yao, Wasije wakaona kwa macho yao, wakafahamu kwa mioyo yao, Wakagenka, nikawaponya.
Sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana mkuu wa ulimwengu anakuja, wala hana kitu kwangu:
Kama singalitenda kazi kwao asizozitenda mtu mwingine, wasingalikuwa na dhambi; sasa wametuona mimi na Baba yangu, na kutuchukia.
Bassi Yesu akanena nao tena, akisema. Mimi ni nuru ya ulimwengu; anifuatae hatakwenda katika giza kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.
uwafumhue macho yao, waiache giza na kuielekea nuru, na waziache nguvu za Shetani na kumwelekea Mungu, na wapate masamaha ya dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwangu.
ya kwamba Kristo hana buddi kuteswa na ya kwamba yeye kwanza kwa kufufuliwa katika wafu atatangaza khabari za nuru kwa watu wake na kwa watu wa mataifa.
Sivyo, lakini vitu vile wavitoavyo mataifi, wavitolea mashetani, wala si Mungu; nami sipendi ninyi kushirikiana na mashetani.
Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu ukomao, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu udumuo.
pamoja na hayo fikara zao zilitiwa ugumu; kwa maana hatta leo utaji huo huo, wakati lisomwapo Agano la Kale, wakaa, haukuondolewa; ambao buoudolewa katika Kristo;
Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiuangalia utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa na kufananishwa na mfano huo huo, toka utukufu hatta utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana aliye Roho.
Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itangʼaa toka gizani, ndive aliyengʼaa mioyoni mwetu, atupe nuru va elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.
aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:
mlizoziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendae kazi sasa katika wana wa kuasi;
Kwa maana shindano letu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza ya ulimwengu huu, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, nae hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa kitu cha kushikamana nacho,
ambao Mungu alipenda kuwajulisha jinsi ulivyo utajiri wa utukufu wa siri hii katika mataifa, nao ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu;
tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Mungu mkuu, Mwokozi wetu Yesu Kristo;
Yeye kwa kuwa ni mwanga wa utukufu wake na chapa ya nafsi yake, akivitengeneza vyote kwa amri ya uweza wake, akiisha kufanya peke yake utakaso wa dhambi zetu, aliketi juu mkono wa kuume wa ukuu;
Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu,
Nasi tuna lile neno la unabii lililo imara zaidi, ambalo, mkiliangalia, kama taa ingʼaayo mahali penye giza, mwafanya vyema, mpaka kutakapopambazuka, na nyota ya assubuhi kuzuka mioyoni mwenu.
Bali yeye amchukiae ndugu yake, yu katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.
Na ile amri ya zamani ndiyo ile mliyosikia tangu mwanzo. Tena nawaandikia amri mpya, neno lililo kweli ndani yake na ndani yenu, kwa kuwa giza linapita na ile nuru ya kweli imekwisha kungʼaa.