Na hayo, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia: kwa maana sasa wokofu u karibu yetu kuliko tulipoamini.
2 Petro 3:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921 Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wahesabuvyo kukawia, bali huvumilia kwenu, hapendi mtu aliye yote apotee, bali wote wafikilie toba. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu. Biblia Habari Njema - BHND Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Bwana hakawii kutimiza yale aliyoahidi kama watu wengine wanavyofikiri kuwa atakawia. Yeye ana saburi kwa ajili yenu, maana hapendi hata mmoja wenu apotee, bali huwavuta wote wapate kutubu. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu hakawii kuitimiza ahadi yake, kama watu wengine wanavyokudhani kukawia. Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba. Neno: Maandiko Matakatifu Mwenyezi Mungu hakawii kuitimiza ahadi yake, kama watu wengine wanavyokudhani kukawia. Badala yake, yeye anawavumilia ninyi, maana hataki mtu yeyote aangamie, bali kila mtu afikilie toba. BIBLIA KISWAHILI Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba. |
Na hayo, tukiujua wakati, kwamba saa ya kuamka katika usingizi imekwisha kuwadia: kwa maana sasa wokofu u karibu yetu kuliko tulipoamini.
Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.
Au waudharau wingi wa wema wake na uvumilivu wake na kusubiri kwake, usijue ya kuwa wema wa Mungu wakuvutia toba?
Bassi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonyesha ghadhabu yake, na kujulisha uweza wake kwa uvumilivu mwingi alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyofanywa tayari kwa uharibifu;
Lakini kwa sababu hii nalirehemiwa, illi katika mimi, wa kwanza, Yesu Kristo adhihirishe uvumilivu wote, niwe mfano kwa wale watakaomwamini baadae, wapate uzima wa milele.
akawakhubiri watu wasiotii hapo zamani, uvumilivu wa Mungu ulipokuwa ukingoja, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ndani yake watu wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji.
kwa hizo tumekarimiwa ahadi kubwa, za thamani, illi kwa hizo mpate kuwa washirika wa sifa za Mungu, mkiokolewa na ubaribifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
Na ubasibuni uvumilivu wa Bwana wetu kuwa wokofu, kama vile na ndugu yetu mpenzi Paolo alivyowaandlkieni kwa hekima aliyopewa;