Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




1 Wakorintho 5:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

Bassi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, illi mwe donge jipya, kama vule mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka yetu amekwisha kutolewa sadaka kwa ajili yetu, yaani Kristo;

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu kama mnavyopaswa kuwa; maana, Kristo, Pasaka yetu, amekwisha tolewa kuwa sadaka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu kama mnavyopaswa kuwa; maana, Kristo, Pasaka yetu, amekwisha tolewa kuwa sadaka.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Jitakaseni, mkatupe mbali chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu kama mnavyopaswa kuwa; maana, Kristo, Pasaka yetu, amekwisha tolewa kuwa sadaka.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu, kama vile mlivyo. Kwa maana Al-Masihi, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kuwa dhabihu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ondoeni chachu ya kale ili mpate kuwa donge jipya lisilotiwa chachu, kama vile mlivyo. Kwa maana Al-Masihi, Mwana-Kondoo wetu wa Pasaka, amekwisha tolewa kuwa dhabihu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Basi, jisafisheni, mkatoe ile chachu ya kale, mpate kuwa donge jipya, kama vile mlivyo hamkutiwa chachu. Kwa maana Pasaka wetu amekwisha kutolewa kuwa sadaka, yaani, Kristo;

Tazama sura
Tafsiri zingine



1 Wakorintho 5:7
19 Marejeleo ya Msalaba  

Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke, akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.


Hatta siku ya kwanza ya mikate isiyochachwa, walipoichinja Pasaka, wanafunzi wake wakamwambia, Wapi unataka tuende tukaandalie uile pasaka?


Siku ya pili yake Yohana amwona Yesu anakuja kwake, akanena, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu, aichukuae dhambi ya ulimwengu!


Akamtazama Yesu, akitembea, akasema, Tazama, Mwana Kondoo wa Mungu!


Ilikuwa Maandalio ya Pasaka: ilikuwa panapo saa sita. Akawaambia Wayahudi, Tazama, mfalme wenu!


ambae Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa damu yake, kwa njia ya imani, illi aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia dhambi zilizotangulia, katika uvumilivu wa Mungu:


Kwa kuwa mkate ni mmoja, sisi tulio wengi tu mwili mmoja; kwa maana sote twapokea sehemu ya ule mkate mmoja.


Bali hao walio nje Mungu atawahukumu. Mwondoeni mtu yule mbaya, asikae kwenu.


mvue kwa khabari ya desturi za kwanza mtu wa zamani, anaeharibiwa kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;


wakisema kwa sauti kuu, Astahili Mwana Kondoo aliyechinjwa kuupokea uweza na utajiri na hekima na nguvu na heshima na utukufu na baraka.