Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya


Zaburi 81 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Swahili Revised Union Version - SRUVDC
Zaburi 81

Ombi la Mungu kwa Waisraeli wakaidi Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Gitithi. Ya Asafu.

1 Mwimbieni Mungu, nguvu zetu, nyimbo za furaha, Mshangilieni Mungu wa Yakobo.

2 Pazeni zaburi, pigeni matari, Kinubi chenye sauti nzuri, na kinanda.

3 Pigeni panda mwandamo wa mwezi, Kukiwa na mbalamwezi, wakati wa sikukuu yetu.

4 Kwa maana ni sheria kwa Israeli, Ni hukumu ya Mungu wa Yakobo.

5 Aliamuru iwe ushuhuda katika Yusufu, Alipoondoka juu ya nchi ya Misri; Maneno yake nisiyemjua niliyasikia.

6 Nimeutua mzigo begani mwake; Mikono yake nikaiondolea kazi nzito.

7 Katika shida uliniita nikakuokoa; Nilikuitikia kutoka maficho yangu ya radi; Nilikujaribu penye maji ya Meriba.

8 Enyi watu wangu, sikieni, nami nitawaonya, Ee Israeli, kama ukitaka kunisikiliza;

9 Usiwe na mungu mgeni ndani yako; Wala usimsujudie mungu mwingine.

10 Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, Niliyekupandisha toka nchi ya Misri; Fumbua sana kinywa chako nami nitakijaza.

11 Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka.

12 Nikawaacha wakaenda kwa ukaidi wa mioyo yao, Waenende katika mashauri yao.

13 Laiti watu wangu wangenisikiliza, Na Israeli angeenenda katika njia zangu;

14 Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu;

15 Wamchukiao BWANA wangenyenyekea mbele zake, Na maangamizi yao yangedumu milele.

16 Naam, ningewalisha kwa ngano iliyo bora zaidi, Ningewashibisha kwa asali itokayo mwambani.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya