Ulinzi wa Mungu kwa mji na watu wake Kwa mwimbishaji. Ya Wakorahi. Kwa mtindo wa Alamothi. Wimbo.1 Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. 2 Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi, Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari. 3 Maji yake yajapovuma na kuumuka, Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake. 4 Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu. 5 Mungu yu katikati ya mji hautatetemeshwa; Mungu atausaidia asubuhi na mapema. 6 Mataifa yanaghadhibika na falme kutetemeka; Anatoa sauti yake, nchi inayeyuka. 7 BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni ngome yetu. 8 Njoni muyatazame matendo ya BWANA, Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi. 9 Avikomesha vita hata mwisho wa dunia; Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari. 10 Tulieni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu, Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi. 11 BWANA wa majeshi yu pamoja nasi, Mungu wa Yakobo ni kimbilio letu. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya