Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya


Zaburi 25 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Swahili Revised Union Version - SRUVDC
Zaburi 25

Sala ya uongozi na ukombozi Zaburi ya Daudi.

1 Ee BWANA, nakuinulia nafsi yangu,

2 Ee Mungu wangu, Nimekutumainia Wewe, nisiaibike, Adui zangu wasifurahi kwa kunishinda.

3 Naam, wakungojao hawataaibika hata mmoja; Wataaibika watendao uhaini bila sababu.

4 Ee BWANA, unijulishe njia zako, Unifundishe mapito yako,

5 Uniongoze katika kweli yako, Na kunifundisha. Maana Wewe ndiwe Mungu wa wokovu wangu, Nakungoja Wewe mchana kutwa.

6 Ee BWANA, kumbuka rehema zako na fadhili zako, Maana zimekuwako tokea zamani.

7 Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.

8 BWANA yu mwema, mwenye adili, Kwa hiyo atawafundisha wenye dhambi njia.

9 Wenye upole atawaongoza katika haki, Wenye upole atawafundisha njia yake.

10 Njia zote za BWANA ni fadhili na kweli, Kwao walishikao agano lake na shuhuda zake.

11 Ee BWANA, kwa ajili ya jina lako, Unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.

12 Ni nani amchaye BWANA? Atamfundisha katika njia anayoichagua.

13 Watafanikiwa maishani mwao; Na wazawa wao wataimiliki nchi.

14 Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.

15 Macho yangu humwelekea BWANA daima, Naye atanitoa miguu yangu katika wavu.

16 Uniangalie na kunifadhili, Maana mimi ni mkiwa na mteswa.

17 Uniondolee shida za moyo wangu, Na kunitoa katika dhiki zangu.

18 Utazame mateso yangu na taabu yangu; Unisamehe dhambi zangu zote.

19 Uwatazame adui zangu, maana ni wengi, Na kwa namna wanavyonichukia kwa ukatili mwingi.

20 Unilinde nafsi yangu na kuniokoa, Usiniache niaibike, maana nakukimbilia Wewe.

21 Ukamilifu na unyofu zinihifadhi, Maana nakungoja Wewe.

22 Ee Mungu, umkomboe Israeli, Katika taabu zake zote.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya