Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya


Zaburi 128 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Swahili Revised Union Version - SRUVDC
Zaburi 128

Nyumba ya mwumini yenye furaha Wimbo wa kupanda mlima.

1 Heri kila mtu amchaye BWANA, Aendaye katika njia yake.

2 Taabu ya mikono yako hakika utaila; Utakuwa heri, na kwako kwema.

3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao, Katika nyumba yako. Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni Wakiizunguka meza yako.

4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.

5 BWANA akubariki toka Sayuni; Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;

6 Naam, ukawaone wana wa wanao. Amani ikae na Israeli.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya