Shukrani kwa kuponywa maradhi1 Haleluya. Nampenda BWANA kwa kuwa anaisikiliza Sauti yangu na dua zangu. 2 Kwa maana amenitegea sikio lake, Kwa hiyo nitamwita siku zangu zote. 3 Kamba za mauti zilinizunguka, Shida za kuzimu zilinipata. Nilipata dhiki na mateso; 4 Nikaliitia jina la BWANA. Ee BWANA, nakuomba sana, Uniokoe nafsi yangu. 5 BWANA ni mwenye neema na haki, Naam, Mungu wetu ni mwenye rehema. 6 BWANA huwalinda wasio na hila; Nilidhilika, akaniokoa. 7 Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu. 8 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti, Macho yangu na machozi, Na miguu yangu na kuanguka. 9 Nitaenenda mbele za BWANA Katika nchi za walio hai. 10 Nilidumisha imani yangu, hata niliposema, Mimi nateseka sana. 11 Nikiwa katika hangaiko langu nikasema, Wanadamu wote ni waongo. 12 Nimrudishie BWANA nini Kwa ukarimu wake wote alionitendea? 13 Nitakipokea kikombe cha wokovu; Na kulitangaza jina la BWANA; 14 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote. 15 Kifo cha waaminifu wa Mungu, kina thamani machoni pa BWANA. 16 Ee BWANA, hakika mimi ni mtumishi wako, Mtumishi wako, mwana wa mjakazi wako, Umevifungua vifungo vyangu. 17 Nitakutolea dhabihu ya kushukuru; Na kulitangaza jina la BWANA; 18 Nitaziondoa nadhiri zangu kwa BWANA, Naam, mbele ya watu wake wote. 19 Katika nyua za nyumba ya BWANA, Ndani yako, Ee Yerusalemu. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya