Nchi zote zaitwa kumsifu Mungu Zaburi ya Shukrani.1 Mshangilieni BWANA, enyi nchi zote; 2 Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake mkiimba; 3 Jueni kwamba BWANA ndiye Mungu; Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake; Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. 4 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake; 5 Maana BWANA ni mwema; Rehema zake ni za milele; Na uaminifu wake katika vizazi vyote. |
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Bible Society of Kenya