Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya


Mwanzo 48 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Swahili Revised Union Version - SRUVDC
Mwanzo 48

Yakobo awabariki wana wa Yusufu

1 Ikawa, baada ya mambo hayo, Yusufu akaambiwa, Tazama, baba yako ni mgonjwa; akawatwaa wanawe wawili, Manase na Efraimu, pamoja naye.

2 Naye Yakobo akaarifiwa ya kwamba, Angalia, mwanao Yusufu anakuja kwako. Israeli akajitia nguvu, akaketi juu ya kitanda.

3 Yakobo akamwambia Yusufu, Mungu Mwenyezi alinitokea huko Luzu, katika nchi ya Kanaani, akanibariki,

4 akaniambia, Mimi hapa, nitakuongezea uzao wako, na kukuzidisha, nami nitakufanya uwe kundi la mataifa; kisha nitawapa wazao wako nchi hii baada yako, iwe milki ya milele.

5 Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.

6 Na wazao wako utakaozaa baada ya hawa watakuwa wako; kwa jina la ndugu zao wataitwa katika urithi wao.

7 Na mimi nilipokuja kutoka Padan, Raheli akanifia katika nchi ya Kanaani, njiani, si mwendo mkubwa kabla ya kufika Efrata. Nikamzika katika njia ya Efrata, ndio Bethlehemu.

8 Israeli akawaona wana wa Yusufu, akasema, Ni nani hawa?

9 Yusufu akamwambia babaye, Hawa ni wanangu, Mungu alionipa nikiwa hapa. Akasema, Tafadhali uwalete kwangu nami nitawabariki.

10 Na macho ya Israeli yalikuwa mazito kwa uzee, wala hakuweza kuona vizuri. Akawaleta kwake, naye akawabusu, na kuwakumbatia.

11 Israeli akamwambia Yusufu, Sikudhani ya kwamba nitakuona uso wako, na Mungu amenionesha na uzao wako pia.

12 Yusufu akawatoa katika magoti yake, naye akainama kifudifudi

13 Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kulia, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kulia wa Israeli, akawasongeza karibu naye.

14 Israeli akanyosha mkono wake wa kulia akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.

15 Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Abrahamu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,

16 naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Abrahamu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.

17 Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kulia juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase.

18 Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kulia kichwani pake.

19 Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa mataifa mengi

20 Akawabariki siku ile akisema, Katika ninyi Waisraeli watabariki, wakisema, Mungu na akufanye kama Efraimu na kama Manase. Akamweka Efraimu mbele ya Manase.

21 Israeli akamwambia Yusufu, Angalia, mimi ninakufa, lakini Mungu atakuwa pamoja nanyi, naye atawarudisha mpaka nchi ya baba zenu.

22 Nami nimekupa wewe sehemu moja zaidi kuliko ndugu zako, niliyoitwaa katika mikono ya Waamori, kwa upanga wangu na upinde wangu.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

Bible Society of Kenya