Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -

Zaburi 71 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Mungu tumaini la wazee

1 Ninakimbilia kwako, ee Yawe, usiniachilie kufezeheka hata kidogo!

2 Kwa haki yako uniokoe na kunikomboa; unitegee sikio lako na kuniokoa!

3 Ukuwe kikingio changu cha kukimbilia, kimbilio lenye nguvu la kuniokoa, kwa maana wewe ni kikingio na kimbilio langu.

4 Uniokoe, ee Mungu wangu, kutoka mikono ya waovu, kutoka makucha ya watu wabaya na wakali.

5 Maana wewe, Bwana wangu Yawe, ni tumaini langu, tegemeo langu tangu ujana wangu.

6 Nimekutegemea tangu kuzaliwa kwangu; wewe ulinilinda nilipotoka katika tumbo la mama yangu. Nitakusifu siku zote.

7 Kwa wengi nimekuwa mushangao, lakini wewe ni kimbilio langu lenye nguvu.

8 Kinywa changu kimejaa sifa zako, na utukufu wako muchana kutwa.

9 Wakati wa uzee usinitupe; ninapoishiwa na nguvu usiniachilie.

10 Maana waadui zangu wanasema vibaya juu yangu; wanaovizia maisha yangu wanafanya mipango,

11 na kusema: “Mungu amemwachilia; mumufuate na kumukamata, kwa maana hakuna wa kumwokoa!”

12 Usikae mbali nami, ee Mungu; ukuje haraka unisaidie, ee Mungu wangu.

13 Wapinzani wangu wote wafezeheke na kuangamizwa; wenye kuvizia kuniua wafezeheke na kuzarauliwa.

14 Lakini mimi nitakuwa na matumaini siku zote; tena nitakusifu zaidi na zaidi.

15 Kinywa changu kitaeleza matendo yako ya haki, nitatangaza muchana kutwa matendo yako ya wokovu ijapokuwa hayo yanapita akili yangu.

16 Nitataja matendo yako makubwa, ee Bwana wangu Yawe; nitatangaza kwamba wewe ndiwe mwenye haki.

17 Ee Mungu, wewe umenifundisha tangu ujana wangu; tena na tena, ninatangaza matendo yako ya ajabu.

18 Usiniachilie, ee Mungu, nitakapokuwa muzee mwenye imvi nyingi, kusudi nivitangazie vizazi vitakavyokuja nguvu yako.

19 Nguvu na haki yako, ee Mungu, vinafika mpaka juu katika mbingu. Wewe umefanya mambo makubwa sana. Ee Mungu, ni nani anayekuwa kama wewe?

20 Umeniletea taabu kubwa, lakini utanirudishia tena uzima, wewe utaniinua tena kutoka katika shimo.

21 Utaniongezea heshima yangu, na kunifariji tena.

22 Nami nitakusifu kwa kinubi, kwa sababu ya uaminifu wako, ee Mungu wangu; nitakuimbia sifa kwa zeze, ewe Mutakatifu wa Israeli.

23 Nitanyanyua sauti kwa furaha, ninapokuimbia wewe sifa zako, na roho yangu itakusifu, maana umeniokoa.

24 Nitatangaza haki yako muchana kutwa, maana wanaonitakia hasara wamefezeheka na kuzarauliwa.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:



ကြော်ငြာတွေ