Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -

Zaburi 5 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Maombi wakati wa hatari

1 Kwa mukubwa wa waimbaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi.

2 Ee Yawe, usikilize maneno yangu, usikie malalamiko yangu.

3 Usikilize kilio changu, Mufalme wangu na Mungu wangu, maana wewe ndiwe ninayekuomba.

4 Ee Yawe, kwa mapambazuko unasikia sauti yangu, asubui ninakutolea sadaka yangu, kisha ninangojea unijibu.

5 Wewe si Mungu anayependa ubaya; mwovu hawezi kupokelewa kwako.

6 Wewe haupendi kuwaona wenye majivuno; wewe unawachukia wote wanaotenda maovu.

7 Unawaangamiza wote wanaosema uongo; unawachukia wauaji na wadanganyifu.

8 Lakini, kwa wingi wa wema wako, mimi nitaingia ndani ya nyumba yako; nitainama kwa heshima kuelekea hekalu lako takatifu.

9 Ee Yawe, katika haki yako, uisawanishe njia yako mbele yangu. Uniongoze kwa sababu ya waadui zangu.

10 Ndani ya vinywa vyao hamuna ukweli wowote; mioyo yao imejaa maangamizi, koo zao ni kama kaburi wazi, ndimi zao zimejaa udanganyifu.

11 Ee Mungu, uwaazibu kwa makosa yao, waanguke katika mipango yao wenyewe; uwafukuze inje kwa sababu ya zambi zao nyingi, kwa sababu wamekuasi wewe.

12 Lakini wanaokimbilia kwako wafurahi wote, waimbe kwa shangwe siku zote. Uwalinde wanaolipenda jina lako, kusudi wapate kushangilia kwa sababu yako.

13 Maana wewe Yawe unawabariki watu wa haki; unawakinga kwa upendo wako kama kwa ngao.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:



ကြော်ငြာတွေ