Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -

Yoshua 21 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Miji ya Walawi

1 Walipokuwa kule Shilo katika inchi ya Kanana viongozi wa ukoo za Walawi wakawaendea kuhani Eleazari na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa jamaa za makabila yote ya Waisraeli,

2 wakawaambia: “Yawe alimwagiza Musa kwamba tupewe miji ya kuishi na mbuga za malisho ya nyama wetu.”

3 Basi, kulingana na amri ya Yawe, Waisraeli walichagua kutoka katika maeneo ya inchi zao, miji na vijiji vya malisho, wakawapa Walawi ikuwe sehemu yao.

4 Kura ya kwanza ilizipata jamaa za ukoo wa Kohati. Kati ya wazao wa kuhani Haruni walipewa kwa kura, miji iliyokuwa katika maeneo ya makabila ya Yuda, Simeoni, na Benjamina. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu.

5 Watu wa ukoo wa Kohati waliobaki wakapewa miji kumi inayokuwa katika maeneo ya makabila ya Efuraimu, Dani na katika eneo la nusu ya kabila la Manase.

6 Watu wa ukoo wa Gersoni wakapewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Aseri, Nafutali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase kule Basani.

7 Jamaa za ukoo wa Merari wakapewa miji kumi na miwili katika maeneo ya makabila ya Rubeni, Gadi na Zebuluni.

8 Waisraeli wakawapa Walawi miji hiyo pamoja na vijiji vya malisho yao, kama Yawe alivyomwagiza Musa.

9 Haya ndiyo majina ya miji kutoka kwenye maeneo ya kabila la Yuda na Simeoni ambayo ilitolewa kwa

10 wazao wa kuhani Haruni, waliokuwa jamaa za ukoo wa Kohati ambaye alikuwa wa kabila la Lawi. Sehemu yao walipata kwanza maana kura yao ilitokea kwanza.

11 Wakapewa Kiriati-Arba, ni kusema Hebroni (Arba alikuwa baba ya Anaki), katika milima ya Yuda, pamoja na mbuga zilizoizunguka.

12 Lakini mashamba ya muji ule pamoja na vijiji vilivyouzunguka vilikuwa vimekwisha kupewa kwa Kalebu mwana wa Yefune vikuwe mali yake.

13 Zaidi ya kuwapa wazao wa kuhani Haruni muji wa Hebroni ambao vilevile ulikuwa umetengwa kuwa muji wa kukimbilia usalama, waliwapa miji ya Libuna pamoja na mbuga zake za malisho;

14 Yatiri pamoja na mbuga zake za malisho, Estemoa pamoja na mbuga zake za malisho,

15 Holoni pamoja na mbuga zake za malisho, Debiri pamoja na mbuga zake za malisho.

16 Aini pamoja na mbuga zake za malisho, Yuta pamoja na mbuga zake za malisho na Beti-Semesi pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji hiyo inayokuwa katika maeneo ya makabila hayo mawili ni tisa.

17 Katika eneo la kabila la Benjamina walipewa miji mingine: Gibeoni pamoja na mbuga zake za malisho,

18 Anatoti pamoja na mbuga zake za malisho, Almoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni mine.

19 Miji yote ya wazao wa Haruni ambao walikuwa makuhani, ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho.

20 Watu waliobaki wa ukoo wa Kohati, ambao vilevile ni watu wa ukoo wa Lawi walipewa miji katika eneo la kabila la Efuraimu.

21 Walipewa Sekemu, muji ambao ulikuwa vilevile muji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho katika inchi ya milima ya Efuraimu, na Gezeri pamoja na mbuga zake za malisho,

22 Kibusaimu pamoja na mbuga zake za malisho na Beti-Horoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni mine.

23 Katika eneo la kabila la Dani walipewa Elteke pamoja na mbuga zake za malisho, Gibetoni pamoja na mbuga zake za malisho,

24 Ayaloni pamoja na mbuga zake za malisho, na Gati-Rimoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni mine.

25 Katika eneo la nusu ya kabila la Manase walipewa Tanaki pamoja na mbuga zake za malisho na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake. Jumla ya miji waliyopewa ni miwili.

26 Basi, miji ambayo walipewa watu wa ukoo wa Kohati iliyobaki ilikuwa kumi pamoja na mbuga zao za malisho.

27 Watu wa uzao wa Lawi wa ukoo wa Gersoni, walipewa miji miwili katika nusu ya eneo la kabila la Manase: Golani, kule Basani, muji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, na Be-Estera pamoja na malisho yake.

28 Katika eneo la kabila la Isakari, walipewa Kisioni pamoja na mbuga zake za malisho, Daberati pamoja na mbuga zake za malisho,

29 Yarmuti pamoja na mbuga zake za malisho na Eni-Ganimu pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni mine.

30 Katika eneo la kabila la Aseri walipewa Misali pamoja na mbuga zake za malisho, Abudoni pamoja na mbuga zake za malisho,

31 Helkati pamoja na mbuga zake za malisho na Rehobu pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni mine.

32 Katika eneo la kabila la Nafutali walipewa Kedesi, muji wa kukimbilia usalama unaokuwa kule Galilaya pamoja na mbuga zake za malisho, Hamoti-Dori pamoja na mbuga zake za malisho na Kartani pamoja na mbuga zake za malisho. Kwa jumla, miji mitatu.

33 Jumla ya miji ya jamaa mbalimbali za ukoo wa Gersoni ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho.

34 Walawi wengine waliobaki, ni kusema wazao wa Merari, walipewa miji katika eneo la kabila la Zebuluni. Nayo ni Yokinamu pamoja na mbuga zake za malisho, Karta pamoja na mbuga zake za malisho,

35 Dimuna pamoja na mbuga zake za malisho na Nahalali pamoja na mbuga zake za malisho. Kwa jumla, miji mine.

36 Katika eneo la kabila la Rubeni walipewa Bezeri pamoja na mbuga zake za malisho, Yahazi pamoja na mbuga zake za malisho,

37 Kedemoti pamoja na mbuga zake za malisho na Mefati pamoja na mbuga zake za malisho. Kwa jumla, miji mine.

38 Katika eneo la kabila la Gadi walipewa Ramoti wa Gileadi, muji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, Mahanaimu pamoja na mbuga zake za malisho,

39 Hesiboni pamoja na mbuga zake za malisho na Yazeri pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mine.

40 Miji yote waliyopewa wazao wa Merari, ni kusema watu wa ukoo wa Walawi zilizobaki, ilikuwa kumi na miwili.

41 Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa makumi ine na nane pamoja na mbuga zao za malisho.

42 Kila mumoja kati ya miji hii ulizungukwa na mbuga za malisho.

43 Basi, Yawe aliwapa Waisraeli inchi yote ambayo alikuwa amewaahidi wazee wao. Nao wakairizi na kuishi mule.

44 Yawe akawapa amani kila pahali katika inchi kama vile alivyowaapia wazee wao. Hakuna adui yeyote aliyesubutu kuwashambulia maana Yawe alikuwa amewatia waadui hao katika mikono yao.

45 Hakuna hata ahadi yoyote njema ambayo Yawe aliiahidi Waisraeli ambayo haikutimia. Ahadi zote zilitimia.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:



ကြော်ငြာတွေ