Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -

Walawi 6 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Sadaka za kuteketezwa kwa moto

1 Yawe akamwambia Musa:

2 Umupatie Haruni na wana wake maagizo haya: hii ndiyo sheria ya ibada juu ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto. Sadaka ya kuteketezwa itakuwa kwenye moto juu ya mazabahu usiku kucha mpaka asubui na moto wake uchochewe, usizimike.

3 Kisha kuhani akiwa amevaa nguo yake ya kitani na kapitula yake ya kitani, atatwaa majivu ya ile sadaka kutoka juu ya mazabahu na kuyaweka kando ya mazabahu.

4 Halafu kisha kubadilisha nguo zake atapeleka yale majivu inje ya kambi pahali panapokuwa safi.

5 Moto wa mazabahu lazima uendelee kuwaka wala usizimike. Kila siku asubui kuhani ataweka kuni kwenye moto huo na juu yake atapanga sadaka ya kuteketezwa, mbele ya kuteketeza mafuta ya sadaka ya amani.

6 Moto utaendelea kuwaka siku zote juu ya mazabahu bila kuzimika hata kidogo.


Sadaka za vyakula

7 Hii ndio sheria juu ya ibada inayoelekea sadaka ya vyakula. Wazao wa Haruni ndio wanaokuwa na uwezo wa kumutolea Yawe sadaka hiyo juu ya mazabahu.

8 Mumoja wa makuhani atatwaa mukono mumoja wa unga wa sadaka ya vyakula pamoja na mafuta na ubani wote na kuviteketeza juu ya mazabahu kama vile sehemu ya ukumbusho. Harufu yake itamupendeza Yawe.

9 Unga uliobakia Haruni na wazao wake makuhani wataukula bila kutiwa chachu. Wataukula kwenye Pahali Patakatifu katika kiwanja cha hema la mukutano.

10 Usipikwe hata kidogo pamoja na chachu. Nimewapa wao sehemu hiyo kutoka sadaka wanazonitolea kwa moto. Ni sadaka takatifu kabisa kama vile sadaka kwa ajili ya zambi na kwa ajili ya kosa zinavyokuwa.

11 Wazao wanaume wa Haruni ndio peke yao wanaoruhusiwa kula sehemu hiyo maana hiyo imetengwa siku zote kwa ajili yao kutoka sadaka Yawe anazotolewa kwa moto. Yeyote atakayezigusa atakuwa mutakatifu.

12 Yawe akamwambia Musa:

13 Tangu wakati wa kutakaswa kwa Haruni na wazao wake wanapaswa kumutolea Yawe kilo moja ya unga laini kwa siku, nusu moja ya unga huo ataitoa asubui na nusu ingine magaribi.

14 Unga huo utachanganywa na mafuta na kupikwa juu ya kikaango. Kisha utauleta ukiwa vipandevipande na kumutolea Yawe na harufu ya sadaka yake itamupendeza Mungu.

15 Kuhani anayekuwa muzao wa Haruni ambaye amepakwa mafuta kushika nafasi yake atamutolea Yawe sadaka hiyo. Hilo ni agizo la milele. Sadaka yote itateketezwa kwa moto.

16 Sadaka yoyote ya ngano iliyotolewa na kuhani itateketezwa yote; haitakuliwa hata kidogo.

17 Yawe akamwambia Musa:

18 Umwambie Haruni na wana wake kwamba hii ndiyo sheria ya ibada kuelekea sadaka kwa ajili ya zambi, pahali ambapo nyama wa sadaka ya kuteketezwa anapochinjiwa ndipo atakapochinjiwa nyama wa sadaka kwa ajili ya zambi, mbele ya Yawe. Hiyo ni sadaka takatifu kabisa.

19 Kuhani anayetolea sadaka hiyo ndiye atakayeikula. Itakuliwa katika Pahali Patakatifu, kwenye kiwanja cha hema la mukutano.

20 Chochote kitakachogusa nyama hiyo kitakuwa kitakatifu. Nguo yoyote ikidondokewa na damu ya sadaka hiyo, basi, nguo hiyo itafuliwa katika Pahali Patakatifu.

21 Sadaka hiyo ikipikiwa katika vyombo vya udongo, vyombo hivyo vitavunjwa. Lakini ikiwa vyombo hivyo ni vya shaba, basi, vitasafishwa vizuri kwa maji.

22 Wanaoruhusiwa kuikula ni wanaume wa ukoo wa makuhani peke yao kwa vile hiyo ni sadaka takatifu kabisa.

23 Lakini kama damu ya sadaka yoyote kwa ajili ya zambi imeletwa ndani ya hema la mukutano kwa kufanya ibada ya upatanisho katika Pahali Patakatifu, sadaka hiyo itateketezwa kwa moto.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:



ကြော်ငြာတွေ