Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -

Walawi 2 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Sadaka za ngano

1 Mutu yeyote akileta sadaka ya ngano kwa Yawe, sadaka hiyo ikuwe ya unga laini. Atautia mafuta na ubani.

2 Kisha, atawaletea hao makuhani, wazao wa Haruni. Atatwaa mukono mumoja wa unga huo laini wenye mafuta na ubani na kumupelekea kuhani mumoja ambaye atauteketeza juu ya mazabahu ukuwe sadaka ya ukumbusho kwa Yawe. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.

3 Sehemu inayobaki ya sadaka hiyo ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.

4 Kama mutu anamutolea Mungu sadaka ya ngano iliyochomwa kwenye furu, hiyo itakuwa ya mikate isiyotiwa chachu ya unga laini uliochanganywa na mafuta ya zeituni, au ya mikate myembamba isiyokuwa na chachu na isiyopakwa mafuta.

5 Ikiwa sadaka unayotoa ni ya mukate uliokaangwa kwenye kikaango, hiyo itakuwa ya unga laini uliochanganywa na mafuta ya zeituni lakini bila chachu.

6 Mikate hiyo itakatwakatwa na kumiminiwa mafuta. Hiyo ni sadaka ya ngano.

7 Kama sadaka unayotoa ni ya mikate iliyopikwa katika sufuria, hiyo itakuwa ya unga laini na imetiwa mafuta.

8 Utaleta sadaka ya ngano iliyotengenezwa kwa vitu hivyo mbele ya Yawe na kuhani ataipeleka kwenye mazabahu.

9 Kuhani atatwaa sehemu ya sadaka hiyo ikiwa ni sadaka ya ukumbusho na kuiteketeza juu ya mazabahu. Hiyo ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto yenye harufu nzuri ya kumupendeza Yawe.

10 Sehemu inayobaki ya sadaka ya ngano, ni ya makuhani. Hiyo ni sehemu takatifu kabisa ya sadaka inayotolewa Yawe kwa moto.

11 Sadaka yoyote ya ngano utakayomuletea Yawe inapaswa kuwa imetengenezwa bila chachu, maana hakuna ruhusa hata kidogo ya kutumia chachu wala asali katika sadaka Yawe anazotolewa kwa moto.

12 Unaweza kumuletea Yawe mazao yako ya kwanza kama sadaka. Lakini hayo hayatatolewa kwenye mazabahu kama harufu ya kumupendeza.

13 Utakoleza sadaka zako zote za ngano kwa chumvi. Usiache hata kidogo kuweka chumvi katika sadaka yako ya ngano, maana chumvi ni kitambulisho cha agano Mungu alilofanya pamoja nanyi.

14 Ukimutolea Yawe sadaka ya mazao yako ya kwanza utaitoa hiyo ikiwa imechomwa katika masuke yake, au utaitoa katika mikate ya kuchomwa iliyotengenezwa kwa ngano iliyosagwa.

15 Utaitia mafuta na kuweka ubani. Hiyo ni sadaka ya ngano.

16 Kuhani atateketeza sehemu ya sadaka hiyo ya ngano iliyopondwa na mafuta pamoja na ubani wake wote, ikuwe sadaka ya ukumbusho. Hiyo ni sadaka Yawe anayotolewa kwa moto.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:



ကြော်ငြာတွေ