Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -

Hosea 11 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002


Upendo wa Mungu unapita hasira yake

1 Israeli alipokuwa mutoto, nilimupenda. Kutoka Misri nilimwita mwana wangu.

2 Lakini kadiri nilivyozidi kuwaita, ndivyo walivyozidi kwenda mbali nami; waliendelea kuyatambikia Mabali, na kuvifukizia ubani sanamu za miungu.

3 Mimi ndiye niliyemufundisha watu wa Efuraimu kutembea! Mimi mwenyewe niliwatwaa katika mikono yangu; lakini hawakutambua kwamba mimi ndiye niliyewatunza.

4 Niliwaongoza kwa huruma, nilishikamana nao kwa upendo; kama baba anavyomunyanyua mutoto mpaka kwenye shavu lake, ndivyo nami nilivyokuwa kwao. Mimi niliinama chini na kuwakulisha.

5 Basi, watarudi katika inchi ya Misri; watatawaliwa na mufalme wa Asuria, kwa sababu wamekataa kunirudilia.

6 Upanga utavuma katika miji yao, utavunjavunja miimo ya milango yake na kuwaangamiza katika kuta zao.

7 Watu wangu wamekusudia kuniacha mimi, wakiitwa kusimama wapande juu, hakuna hata mumoja anayeweza.

8 Ewe Efuraimu, ninaweza kukuacha namna gani? Ninaweza kukutupilia, ewe Israeli namna gani? Nitaweza namna gani kukufanya kama muji wa Adama? Nitaweza namna gani kukutendea kama Zeboimu! Ninazuizwa na moyo wangu; huruma yangu imezidi kuwa motomoto.

9 Nitaizuia hasira yangu kali; sitamwangamiza tena Efuraimu, maana mimi ni Mungu, wala si mwanadamu. Mimi ndimi Mutakatifu kati yenu, nami sitakuja kuwaangamiza.

10 Watanifuata mimi Yawe ninayenguruma kama simba; nitakaponguruma watanifikia toka magaribi wakitetemeka.

11 Watakuja kutoka Misri wakitetemeka kama ndege, wataruka kutoka Asuria kama njiwa nami nitawarudisha kwao. –Ni ujumbe wa Yawe.

Bible in Swahili Congo © Bible Society of the Democratic Republic of Congo (DRC), 2002.

Bible Society of the Democratic Republic of Congo
ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:



ကြော်ငြာတွေ