Niko wikacha wikawiwanga walindiri wa mbenge ya muzi, wikawighoria wikighamba, “Dereghendieghe kambinyi ya Wasiria, ela ndediwonie hata kusikira mndungi, ela deekua farasi rifungie, na punda na hema rasighwa kimusi sa iji koni riko.”
Walindiri mbenge ni awa: Kivalwa cha Shalumu, na cha Ateri, na cha Talmoni, na cha Akubu, na cha Hatita, na cha Shoibai, ighana mirongo idadu na wunyanya.
Kusinda Hekalunyi kwako ituku jimweri, kwachumba matuku elfu andu kuzima. Ni baa kukaia mlindiri wa mnyango ghwa nyumba ya Mlungu wapo, kuchumba kukaia andenyi ya mizi ya wandu wawiwi.