2 Ee Mungu, uniokoe! Ee Yawe, ukuje haraka unisaidie.
Waadui zangu wazungukwe na mazarau; wajifunike haya yao kama vile nguo.
Kwa mukubwa wa waimbaji: Zaburi ya Daudi. Ninakulilia, ee Yawe, ukuje haraka kunisaidia! Usikilize sauti yangu wakati ninapokuita!
Usikae mbali nami, kwa maana taabu imekaribia; wala hakuna wa kunisaidia.
Lakini wewe, ee Yawe, usikae mbali nami. Ukuwe musaada wangu, ukuje haraka kunisaidia.
Uwaache hao wanaofurahia hasara yangu, washindwe wote na kufezeheka. Hao wote wanaojiona bora kuliko mimi, wapate haya na kufezeheka.
Wapate haya na kuzarauliwa, hao wanaotaka kupoteza maisha yangu! Warudishwe nyuma na kufezeheka, hao wanaonitafutia hasara.
Upendezwe, ee Yawe, kuniokoa; ee Yawe, ukuje haraka kunisaidia.
Yawe amesikia ombi langu; Yawe amekubali maombi yangu.
Usikae mbali nami, ee Mungu; ukuje haraka unisaidie, ee Mungu wangu.
Wapinzani wangu wote wafezeheke na kuangamizwa; wenye kuvizia kuniua wafezeheke na kuzarauliwa.
Basi Yawe atawafundisha kama watoto wadogo: kanuni juu ya kanuni, mustari juu ya mustari; mara hiki, mara hiki! Nao watalazimishwa kukimbia lakini wataanguka machalichali, watavunjika, watanaswa na kutekwa.
Kweli! Wote waliokukasirikia, watapata haya na kufezeheka. Wote wanaopingana nawe, watakuwa wa bure na kuangamia.
Yesu alipowaambia: “Ni mimi,” wakarudi nyuma na kuanguka.