Lakini sikuweza kuamini habari hizo mpaka nilipofika na kujionea mwenyewe. Kumbe sikuambiwa hata nusu yake; hekima yako na fanaka zako vimepita habari nilizopewa.
Unipeleke, tuende haraka, mufalme amenileta katika chumba chake. Tutafurahi na kukushangilia pamoja, tutasifu mapenzi yako kuliko divai. Wabinti wana haki ya kukupenda!
Bonde lote walimozikwa wafu na kutupiwa majivu, mashamba yote, mpaka kijito cha Kidroni, mpaka pembe ya mulango wa Farasi kuelekea upande wa mashariki, litakuwa eneo takatifu kwa Yawe. Hakuna kitakachoharibiwa humo wala kubomolewa tena milele.