Kisha waliliingiza Sanduku la Yawe ndani ya hema ambalo Daudi alikuwa amelisimamisha pale na kuliweka pahali pake. Naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele ya Yawe.
Chumba cha ndani, kilichoitwa Pahali Patakatifu Sana, kilijengwa katika sehemu ya nyuma ya nyumba. Kilikuwa kimejengwa kwa mbao za mierezi kutokea kwenye sakafu mpaka kwenye dari, na urefu wake ulikuwa metre tisa.