5 Nimefuata siku zote njia yako; wala sijatereza hata kidogo.
Hayo yote yametupata sisi ijapokuwa hatujakusahau, wala hatujavunja agano lako.
Uniimarishie hatua zangu kama ulivyoahidi; usikubali mimi nitawaliwe na uovu.
Yawe atakukinga na uovu wote; atayalinda salama maisha yako.
Hatakuacha uanguke; mulinzi wako hasinzii.
Lakini ninakutumainia wewe, ee Yawe; wewe, ee Yawe, Mungu wangu, ndiwe utakayenijibu.
Umenipa ngao yako ya wokovu na kuniimarisha kwa mukono wako wa kuume. Nimefanikiwa kwa sababu ulikubali kunisaidia.
Nilipotambua kwamba ninateleza, wema wako, ee Yawe, ulinikingia.
Anayalinda maisha ya waaminifu wake, lakini anaangamiza maisha ya waovu katika giza. Maana, mwanadamu hapati ushindi kwa nguvu zake.
Ninajua, ee Yawe, mwanadamu hana uwezo juu ya maisha yake; hakuna mutu anayeweza kuongoza maisha yake.
Ninamufuata kabisa; njia yake nimeishikilia wala sikugeuka pembeni.
Umepanua njia yangu wala miguu yangu haikuteleza.