Biblia Todo Logo
အွန်လိုင်း သမ္မာကျမ်းစာ

- ကြော်ငြာတွေ -




Yoshua 7:24 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002

24 Yoshua pamoja na Waisraeli wote, wakamukamata Akana mwana wa Zera, pamoja na feza, nguo, zahabu, watoto wake wa kiume na wabinti zake, ngombe, punda na kondoo wake, hema lake na kila kitu alichokuwa nacho na kuwapeleka kwenye bonde la Akori.

အခန်းကိုကြည့်ပါ။ ကော်ပီ




Yoshua 7:24
18 ပူးပေါင်းရင်းမြစ်များ  

Sizani kama utafanya hivyo, kuwaua watu wa haki pamoja na waovu, kutendea watu wa haki sawa na waovu. Hapana, haiwezekani! Mwamuzi wa dunia yote hataacha kutenda mambo yanayokuwa sawa!”


Mwovu anameza mali haramu na kuitapika; Mungu anaitoa ndani ya tumbo lake.


Usiiname mbele yao wala kuvitumikia, kwa sababu mimi Yawe, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu. Ninawaazibu wana kwa ajili ya maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha ine cha wale wanaonichukia.


Anayetamani faida ya unyanganyi anataabisha jamaa yake, lakini anayechukia kituliro ataishi.


Kwa bahati mbaya, mali hiyo iliharibiwa katika matumizi mabaya. Kwa mwisho, mutu yule hakukuwa na kitu chochote wakati alipokuwa na mwana.


Bonde la Saroni litakuwa nafasi ya kukulishia nyama, bonde la Akori litakuwa mapumziko ya ngombe kwa ajili ya watu wangu walionitafuta.


Nitamulipiza kwa ajili ya siku alizoabudu sanamu za mungu Bali, kwa ajili ya muda alioutumia kuzifukizia ubani, akajipamba kwa pete zake na ushanga, na kuwaendea wapenzi wake, akanisahau mimi. –Ni ujumbe wa Yawe.


Kutoka hapo, uliendelea mpaka Debiri kwenye bonde la Akori na kaskazini kuelekea Gilgali, karibu na mwinuko wa Adumimu ambao uko upande wa kusini wa kijito, kisha ukaelekea kwenye chemichemi za Eni-Semesi na kuishia Eni-Rogeli.


Akana mwana wa Zera alipokosa uaminifu katika vitu vitakatifu, kasirani haikuangukia Waisraeli wote pamoja? Tena Akana hakukufa tu yeye peke yake kwa sababu ya uovu wake.’ ”


Lakini musitwae kitu chochote ambacho kimetolewa kusudi kiangamizwe. Mukitwaa kitu chochote ambacho kimetolewa kusudi kiangamizwe, mutaifanya kambi ya Israeli kuwa kitu cha kuangamizwa, na hivyo kuiletea hasara.


Kisha wakaangamiza kila kitu katika muji ule na kuwaua kwa upanga: wanaume na wanawake, vijana na wazee, ngombe, kondoo na punda.


Lakini Waisraeli hawakukuwa waaminifu juu ya vile vitu vilivyotolewa viangamizwe maana Akana mwana wa Karmi, mujukuu wa Zabedi, wa ukoo wa Zera, wa kabila la Yuda, alitwaa vimoja kati ya vitu vilivyoamriwa viteketezwe. Kwa hiyo hasira ya Yawe ikawaka juu ya Waisraeli.


Wakavitwaa toka katika hema na kuvipeleka kwa Yoshua na watu wote wa Israeli; nao wakaviweka chini, mbele ya Yawe.


Halafu wakalundika mawe mengi juu yake, ambayo yako mpaka leo. Hapo hasira ya Yawe ikapoa; na pahali pale pakaitwa Bonde la Akori, ni kusema Bonde la Taabu, mpaka hivi leo.


ကြှနျုပျတို့နောကျလိုကျပါ:

ကြော်ငြာတွေ


ကြော်ငြာတွေ