Basi, kesho yake, Abrahamu akaamuka asubui mapema, akatandika punda wake, akawatwaa watumishi wake wawili pamoja na Isaka mwana wake. Akatayarisha kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa moto, kisha akaanza safari kuelekea pahali alipoambiwa na Mungu.
Asubui mapema Yoshua pamoja na watu wote wa Israeli walianza safari kutoka Sitimu. Walipofika kwa muto Yordani, walipiga kambi hapo kwa muda mbele ya kuvuka.
Mutu yeyote atakayepatikana akiwa na vitu vilivyotolewa viangamizwe atateketezwa kwa moto, yeye pamoja na kila kitu chake maana ameliasi agano langu mimi Yawe, akatenda jambo la haya katika Israeli.’ ”
Akazileta karibu ukoo za Yuda, ukoo kwa ukoo; na ukoo wa Zera ukachaguliwa. Akazileta karibu jamaa za ukoo wa Zera, jamaa kwa jamaa; na jamaa ya Zabedi ikachaguliwa.