Yoshua 6:1 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 20021 Milango ya kuingilia katika muji wa Yeriko ilikuwa imefungwa imara kwa ndani kwa kuwazuia Waisraeli wasiingie. Hakuna mutu aliyeweza kuingia wala kutoka katika muji huo. အခန်းကိုကြည့်ပါ။ |
Miji ya ukoo za kabila la Benjamina ni: Yeriko, Beti-Hogla, Emeki-Kesisi, Beti-Araba, Zemaraimu, Beteli, Awimu, Para, Ofura, Kefari-Amoni, Ofuni na Geba. Jumla ya miji kumi na miwili pamoja na vijiji vyake. Gibeoni, Rama, Beroti, Misipa, Kefira, Moza, Rekemu, Iripeli, Tarala, Zela, Ha-Elefu, Yebusi, ni kusema Yerusalema, Gibea na Kiriati-Yearimu. Jumla ya miji kumi na mine pamoja na vijiji vyake. Hiyo yote ni sehemu watu wa kabila la Benjamina na ukoo zao waliyopewa.