Musa akawapeleka kwa vita chini ya uongozi wa Finehasi mwana wa kuhani Eleazari, akiwa na vyombo vya Pahali Patakatifu na baragumu za kutoa kitambulisho.
Finehasi mwana wa Eleazari mwana wa Haruni alikuwa na kazi ya kutumika mbele yake. Waisraeli wakamwuliza Yawe: “Twende tena kupigana na wandugu zetu, watu wa kabila la Benjamina?” Yawe akawaambia: “Muende. Kesho nitawatia katika mikono yenu.”