Nao Edeni, Miniamini, Yesua, Semaya, Amaria na Sekania, walimusaidia kufanya kazi hiyo kwa uaminifu katika ile miji mingine makuhani walimoishi. Waliwagawanyia wandugu zao Walawi vyakula, kwa wakubwa kama vile kwa wadogo.
Kura ya kwanza ilizipata jamaa za ukoo wa Kohati. Kati ya wazao wa kuhani Haruni walipewa kwa kura, miji iliyokuwa katika maeneo ya makabila ya Yuda, Simeoni, na Benjamina. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu.