Jamaa za Merari zilizobakia, zilipewa miji hii pamoja na mashamba yake ya malisho kandokando ya miji hiyo. Katika kabila la Zebuluni walipewa Rimono pamoja na mashamba yake ya malisho na Tabori pamoja na mashamba yake ya malisho.
Katika kabila Rubeni, upande wa mashariki ya muto Yordani karibu na muji wa Yeriko walipewa Bezeri unaokuwa katika inchi ya vilima pamoja na mashamba yake ya malisho, Yahasa pamoja na mashamba yake ya malisho,
Watu wa ukoo wa Gersoni wakapewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Aseri, Nafutali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase kule Basani.