Yoshua 21:5 - BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002
5 Watu wa ukoo wa Kohati waliobaki wakapewa miji kumi inayokuwa katika maeneo ya makabila ya Efuraimu, Dani na katika eneo la nusu ya kabila la Manase.
Katika kabila la Nafutali: Kedesi katika Galilaya pamoja na mashamba yake ya malisho, Hamoni pamoja na mashamba yake ya malisho na Kiriataimu pamoja na mashamba yake ya malisho.
Kura ya kwanza ilizipata jamaa za ukoo wa Kohati. Kati ya wazao wa kuhani Haruni walipewa kwa kura, miji iliyokuwa katika maeneo ya makabila ya Yuda, Simeoni, na Benjamina. Jumla ya miji waliyopewa ni kumi na mitatu.
Watu wa ukoo wa Gersoni wakapewa kwa kura miji kumi na mitatu katika maeneo ya makabila ya Isakari, Aseri, Nafutali na katika eneo la nusu ya kabila la Manase kule Basani.