40 Miji yote waliyopewa wazao wa Merari, ni kusema watu wa ukoo wa Walawi zilizobaki, ilikuwa kumi na miwili.
Hesiboni pamoja na mbuga zake za malisho na Yazeri pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla miji mine.
Jumla ya miji yote ambayo Walawi walipewa katika maeneo ya Waisraeli ilikuwa makumi ine na nane pamoja na mbuga zao za malisho.
Jamaa za ukoo wa Merari wakapewa miji kumi na miwili katika maeneo ya makabila ya Rubeni, Gadi na Zebuluni.