Katika eneo la nusu ya kabila la Manase walipewa Tanaki pamoja na mbuga zake za malisho na Gati-Rimoni pamoja na malisho yake. Jumla ya miji waliyopewa ni miwili.
Watu wa uzao wa Lawi wa ukoo wa Gersoni, walipewa miji miwili katika nusu ya eneo la kabila la Manase: Golani, kule Basani, muji wa kukimbilia usalama, pamoja na mbuga zake za malisho, na Be-Estera pamoja na malisho yake.