20 Watu waliobaki wa ukoo wa Kohati, ambao vilevile ni watu wa ukoo wa Lawi walipewa miji katika eneo la kabila la Efuraimu.
Jamaa zingine za ukoo wa Kohati zilipewa miji pamoja na malisho yake katika kabila la Efuraimu:
Hesiboni pamoja na mashamba yake ya malisho na Yazeri pamoja na mashamba yake ya malisho.
Miji yote ya wazao wa Haruni ambao walikuwa makuhani, ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho.
Watu wa ukoo wa Kohati waliobaki wakapewa miji kumi inayokuwa katika maeneo ya makabila ya Efuraimu, Dani na katika eneo la nusu ya kabila la Manase.