19 Miji yote ya wazao wa Haruni ambao walikuwa makuhani, ilikuwa kumi na mitatu pamoja na mbuga zao za malisho.
Katika kabila la Isakari walipewa: Kedesi pamoja na mashamba yake ya malisho, Deberati pamoja na mashamba yake ya malisho,
Anatoti pamoja na mbuga zake za malisho, Almoni pamoja na mbuga zake za malisho. Jumla ya miji waliyopewa ni mine.
Watu waliobaki wa ukoo wa Kohati, ambao vilevile ni watu wa ukoo wa Lawi walipewa miji katika eneo la kabila la Efuraimu.